WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuangalia filamu zinazozalishwa na wasanii wa ndani, ili waweze kuzikosoa na kupata zenye ubora utakaokidhi soko la kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa filamu ya The Green Tanzanite , Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa, amesema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuzipa kipaumbele filamu zinazozalishwa hapa nchini ili waweze kutoa tathmini ya ubora wa filamu.
“Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakizipa kipaumbele filamu za nje, ifike wakati Watanzania wakuze utamaduni wa kuziangalia filamu zao ili waweze kuzikosoa, ” amesema Ndumukwa.
Kwa upande wake mzalishaji wa filamu ya The Green Tanzanite, Salma Bhamra amesema kuwa baadhi ya wasanii wa Tanzania katika sekta ya filamu wabafanya vizuri, lakini wamekuwa wakikosa hamasa jambo linalowakatisha tamaa.
Amesema katika nchi za Afrika Kusini na Nigeria, wamekuwa wakipata hamasa kutoka kwa mashabiki na hata pia serikali zao.
Naye Mwakilishi wa Century Cinema, Shahzaib Jafar amesema kuwa filamu nyingi za Tanzania ni nzuri, lakini zimekosa watu wa masoko katika kuzihamasisha.
Comments are closed.