‘Watalii 35,562 walitembelea hifadhi za bahari’

SERIKALI imesema hadi kufikia Aprili, 2023 watalii 35,562 walitembelea Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema kiasi cha shilingi bilioni 1.68 kilikusanywa ikilinganishwa na watalii 22,562 na shilingi bilioni 1.18 zilizokusanywa mwaka 2021/2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 42.4 la mapato yatokanayo na utalii.

Habari Zifananazo

Back to top button