HIFADHI ya Taifa Ruaha imeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na kuwa na vivutio vya kila aina hususani makundi ya Simba katika familia moja zaidi ya 40, utalii wa usiku na mchana, hali inayosababisha mtalii kukaa siku zaidi ya moja hifadhni humo.
Akizungumzia Hifadhi hiyo, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng’ataki, amesema hifadhi hiyo imekuwa kimbilio la watalii wengi kutokana na utajiri wa vivutio kwenye hifadhili, malazi, vyakula vya bei rafiki na hata uvuvi wa kitalii.
Ameongeza kuwa hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa nchini, imekuwa kivutio kikubwa kutoka kuwa na miundombinu mizuri hususani barabara ndani ya hifadhi kupitia mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).
Kamishna huyo amesema kupitia Mradi huo wa REGROW, Hifadhi hiyo inatekeleza ujenzi wa kiwanja cha ndege, barabara ndani ya hifadhi, uchimbaji wa mabwawa 32 kwa ajili ya wanyamapori, ujenzi wa sehemu za malazi, kituo cha Utafiti, kwa ajili ya ulinzi wa Maliasili.
Kuhusu hifadhi hiyo, na namna alivyo furahia utalii, Mtalii kutoka Ufaransa Ines Richard, amesema imekuwa ni zaidi ya matarajio kwa kuwa licha ya kuona makundi makubwa ya Simba, pia ameweza kuona Wanyama wakubwa na wadogo, ndege zaidi ya aina 570 na mimea ya kila aina.
Amesea utalii wa miguu ndani ya hifadhi ni kivutio pia Kwa Kila mtalii kwani anaweza kuona hata kile ambacho hakutarajia.
Comments are closed.