JESHI la Polosi mkoani Arusha limezifungia leseni tano za udereva kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema.
Leseni hizo zimefungiwa kwa kati ya miezi mitatu na sita. Masejo ametaja makosa yaliyopelekea hatua hiyo ni kuwa ni pamoja na ulevi, mwendokasi, kusababisha ajali, wenye makosa yanayojirudia pamoja na wale ambao wanayapita magari mengine (overtaking) sehemu ambazo zimekatazwa kisheria.
Kamanda Masejo amebainisha kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kutoa elimu katika nyumba za ibada, stendi za mabasi, mashuleni, vijiwe vya bodaboda pamoja na masoko ambapo jamii hiyo imepata uelewa wa kutosha kuhusiana na sheria mbalimbali za usalama barabarani.
Polisi imeonya madereva wanaoendele kuvunja sheria za usalama barabarani ikisisitiza kuchukua hatua kali kwa dereva yeyote atakaye kutwa na hatia ya kuvunja sheria za usalama barabarani.