Watano wasimamishwa kazi kifo cha mjamzito Tanga
TANGA:Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amemuagiza Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Dk. Frederick Sagamiko kuwasimamisha kazi watumishi wa afya watano kutokana na uzembe uliosababisha kifo cha mama mjamzito muda mchache baada ya kujifungua.
Amewataja watumishi hao ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Hoza, Restituta Deusdedit na Muya Mohamed, madaktari waliofanya upasuaji Andrew Kidee na Hamis Mohamed.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema kuwa Marehemu Fatuma Suleiman (36) alifika katika kituo cha afya Mikanjuni Machi 27 saa 10 alfajiri kwa tatizo la uchungu na baada ya kujifungua ndipo alipoongezewa damu pasipo na uhitaji na kupelekea kupata mzio mkali ambao uliosababisha kifo chake