‘Watanzania changamkieni fursa uwekezaji madini’
WATANZANIA watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishina wa Madini Dk Abdulrahman Mwanga ameeleza kuwa, uwekezaji katika madini si lazima uwe mchimbaji, bali unaweza kutoa huduma mbalimbali.
“Kuwekeza kwenye sekta ya madini sio kwa mchimbaji tu, kuna huduma mbalimbali, unaweza kutoa kama usambazaji wa chakula, vifaa vya migodini, utoaji wa haki za kisheria kwa watu wa migodini.
“Unaweza kuwekeza katika kutoa taaluma yako kama ni mwanasheria kwa kutoa msaada wa kisheria, tusilale, tuchangamkie hizi fursa,” amesema Dk Mwanga.