Watanzania mil.8.5 kufikiwa mawasiliano

MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema Watanzania milioni 8.5 watafikiwa na huduma za mawasiliano baada ya kukamilika ujenzi wa minara 758, katika Mikoa 26, Wilaya 127, Kata 713 na Vijiji 1,407 vya Tanzania Bara.

Akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo, Mei 13, 2023, Justina amesema tukio hilo ni la kihistoria kwa taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button