Watanzania waliopo Israel kurejeshwa nchini

DODOMA: SERIKALI imewataka watanzania waliopo nchini Israel kuwiwa kujiandikisha katika ubalozi wa Tanzania uliopo Tel Aviv ili kurejeshwa nchini.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iiliyotolewa kwa umma na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo, jijini Dodoma.

“Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo,” imedokeza taarifa hiyo ya wizara.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mawasiliano inabidi yafanyike kabla ya Oktoba 15, 2023, saa 6 usiku kupitia ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Israel, kupitia barua pepe: telaviv@nje.go.tz au namba ya simu +972533044978 na +972507650072.

Habari Zifananazo

Back to top button