Watanzania wang’ara Kilimanjaro Marathon

WANARIADHA watanzani wameiheshimisha nchi baada ya kung’aa katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MUCCOBS) mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro leo.

Kwa upande wa wanaume Mtanzania, Sulle Augostino ameibuka mshindi wa mbio za kilometa 42 baada ya kukimbia kwa muda wa saa 2: 21:06, akifuatiwa na Abraham Too aliyekimbia saa 2:22:02 na nafasi ya tatu amechukua Elisha Kimijtai aliyetumia saa 2: 22: 17 wote raia wa Kenya.

Kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza imeenda kwa Mtanzania, Natalia Sulle aliyetumia saa 2:51:23 nafasi ya pili Neema Sanka, nafasi ya tatu Vailet Kidasi, nafasi ya nne, Mary Naali, nafasi ya tano, Angelina Yumba na nafasi ya sita, Catherine Yuku wote watanzania.

Advertisement

Katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume, nafasi ya kwanza imeenda kwa Mtanzania, Faraja Lazaro aliyetumia saa 1:03:33 na kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza imeenda kwa Mtanzania, Failuna Matanga aliyetumia saa 1:16:40