Watanzania wapewa ofa wakajifunze Kirusi

CHUO Kikuu cha St Petersburg cha nchini Urusi kimetoa ofa maalum kwa Watanzania kujifunza lugha hiyo bila malipo.

Taarifa ya chuo hicho imeeleza kuwa programu hiyo inaratibiwa na Wizara ya Elimu nchini Urusi ni maalum kwa Watanzania kusoma nchini humo, ambapo watajifunza pia lugha hiyo, ili kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uchumi, hatua inayoongeza nafasi kwa Watanzania kufanya kazi Urusi na Warusi kufanya kazi Tanzania.

Taarifa imeeleza kuwa  chuo kikuu hicho kikongwe zaidi nchini Urusi kimekuwa kikitoa programu mbalimbali za kielimu na kitamaduni.

Chuo hicho kimeeleza kuwa Agosti 15 na 16, lilifanyika tamasha la Utamaduni wa Kirusi katika kituo cha utamaduni cha Urusi jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki zaidi 200 walihudhuria.

Kupitia tamasha hilo, walijionea tamadani mbalimbali za Kirusi ikiwemo mikate, ngoma na kufundishwa namna ya kusaini kadi za posta za Kirusi kutoka kwa mtaalamu Khokhloma.

Taarifa hiyo inasema kuwa tamasha hilo la Kirusi linatarajiwa kufanyika pia Zanzibar na Arusha, ambapo wafanyakazi wa utalii wanasisitizwa kuchangamkia ofa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button