Watanzania watakiwa kutumia fursa sio kulalamika

WAKATI kampuni  266 za kimataifa zikishiriki  Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Baishara ‘Sabasaba’ watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara badala ya kuishia kulalamika.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akizungumza leo Julai 4, 2023 katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ ikiwa ni siku ya taifa la China amesema ni fursa  kwa watanzania kutembelea banda la wachna ili  kujenga mtandao wa kirafiki na kampuni hizo na  kufanya nao biashara.

“Wanaokuja kwenye maonyesho haya wasiache  kuingia banda la uchina kujifunza teknolojia mbali mbali pia wahakikishe wanajenga mtandao mzuri wa ushirikiano, kuwashawishi kufungua makampuni yao hapa na kuzalisha bidhaa hapa nchini badala ya kufuata China,”amesema na kuongeza

“Tanzania iwe ufunguo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ili uchumi wa Tanzania  ukue. Watanzania wasiishie kulalamika wachina wamechukua kazi zao, masoko yao, waungane nao.”Amesema

Amesema, katika kampuni 266 zilizoshiriki zaidi ya kampuni 100 ni za kutoka China na kampuni moja wapo ni ya  East African Commercial and Logistics Center inayojenga mradi wa mkubwa wa soko Ubungo na ndio mdhamini mkuu wa maonesho ya mwaka huu.”Amesema Kigahe na kuongeza

“China ni washirika wakubwa wa Tanzania  katika bidhaa mbali mbali kama tiles na bidhaa nyingi za majumbani,  kampuni  zilizotoka China kuwekeza ni mengi.

“Mwaka jana China ilichukua eneo sababsaba la square mita 400 lakini mwaka huu wamechukua square mita 500 peke yao.”Amesema na kuongeza

“Wachina pia wametumia ndege ya Air Tanzania zaidi ya mara 52 kuja kwenye maonyesho haya maana yake nini wameongeza uchumi kupitia ATCL.”Amesema

Amesema, Makampuni ambayo yamewekeza hapa wengine unganisha trekta na mabegi na kwamba kampuni za China yataenda kuongeza thamani ya bidhaa zaidi

Kwa upande wake meneja wa EACLC inayodhamini maonesho ya sabasaba, Wang Xiangyu amesema kuwa kampuni zilizokuja kutoka china kuhudhuria maonesho ya sabasaba wamekuja kutambulisha kampuni zao jambo ambalo litaendeleza ushirikiano mzuri kwa nchi zote mbili na hivi sasa maonesho ya sabasaba ni maarufu sana kule china hivyo wanaamini  watu wengi watafika kutembelea banda la China.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button