Watanzania watatu waokolewa meli iliyozama DRC

DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limesema watu 17 wameokolewa katika tukio la kuzama Meli ya MV Maman Benita kwenye Ziwa Tanganyika, iliyokuwa inatoka Kigoma kuelekea Kalemie nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ikiwa na Abiria 27, Aprili 6, 2024

Taarifa ya TASAC imesema April 7,2024 wavuvi walifanikiwa kumwokoa abiria mmoja mwenye asili ya China na kisha walitoa taarifa kwa Mamlaka za Serikali za DRC juu ya kuzama kwa meli hiyo

TASAC imesema baada kupata taarifa ya meli hiyo ukoaji ulianza mara moja hadi kufikia saa 1:00 usiku wa Aprili 7 waathirika 17 waliokolewa kati yao ikijumuisha wachina wawili, Watanzania watatu na Wakongo 12.

Taarifa imesema chanzo cha kuzama kwa meli hiyo bado hakijajulikana isipokuwa nahodha wa meli hiyo ameokolewa na timu ya wataalamu imeenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji

Habari Zifananazo

Back to top button