Watendaji Mtwara watakiwa kuwajali wengine

WATENDAJI kutoka halmashauri mbalimbali mkoani Mtwara wametakiwa kuwajali watendaji walio chini na juu yao ili kukamilisha malengo yanayokusidiwa kwenye mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas katika kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Mtwara mwaka 2024 (RCC).

Advertisement

Kikao hicho kimefanyika leo Machi 5, 2024 mkoani humo chenye lengo la kujadili Ajenda moja maalum kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa nusu mwaka wa fedha 2023/24.

Hata hivyo makadilio ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 kabla ya kuwasilishwa kwenye ngazi zinazofata kwa mujibu wa sheria, itayotekelezwa katika halmashauri zote 9 mkoani humo.

Kanali Ahmed Abbas amesema pamoja na majadiliano hayo lakini yapo mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji huo.

“Tutumie kikao hiki kujadili na kutoa ushauri utakao saidia kuboresha mipango na bajeti zetu, haya yanaweza kufanikiwa endapo tu tutakuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu”

Aliongeza kuwa “Kama tutawajali watu walioko chini yetu na walioko juu yetu ikiwa mnaweza kutofautiana kwenye mitizamo lakini kwenye kujali maslahi ya watu, utu wa watu hivi vitu vikifanyika vizuri vinatufanya sote kufanya kazi kwa ushirikiano ili mwisho wa siku tuweze kukamilisha malengo haya tunayo yasema,”amesema Abbas

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuzye amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili mkoa huo wakati wa utekelezaji wa bajeti hizo ikiwemo kuchelewa kufika kwa fedha za ruzuku ya miradi ya maendeleo.