Watendaji wa vijiji chanzo cha mapigano wakulima, wafugaji

DC atoa siku 14 kwa Mkurugenzi

WAFUGAJI wa halmashauri za wilaya za Chalinze na Bagamoyo, mkoani Pwani, wamewatuhumu baadhi ya viongozi wa vijiji kuwa sehemu ya migogoro kati yao na wakulima kutokana na kuhodhi na kuuza maeneo yaliotegwa kwa ajili ya malisho ya mifugo kwa wawekezaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkuatano wa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash wa kusikiliza kero za wafugaji hao, wamesema mapigano kati yao na wakulima yamekuwa yakichochewa na viongozi wa vijiji kutokana na kuuza maeneo ya malisho kwa wawekezaji kinyume na taratibu.

Mwenyekiti wa Chama Cha wafugaji, Halmashauri ya Chalinze,amesema baadhi ya viongozi wamehusika kuuza maeneo yaliotegwa kwa ajili ya wafugaji ikiwemo yale yalioingizwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Amesema, baadhi ya viongozi wa vijiji waliouza maeneo hayo ni kijiji cha Kikaro, Magulumatari,Mkenge na kijiji cha Kiwagwa na kwamba viongozi hao hawatambui mpango wa matumizi bora ya ardhi.

“Viongozi hawatambui mpango wa matumizi Bora ya ardhi na kuuza maeneo yetu ikiwemo kusababisha migogo ya mipaka ya vijiji vya wafugaji.”Amesisitiza

Naye Mwenyekiti wa wafugaji Halmashauri ya Bagamoyo, Alex Masha,amesema wafugaji wamekuwa wakipokonywa maeneo yao bila kulipwa fidia na kutopewa maeneo mengine mbadala.

Aidha, amesema changamoto nyingine ni kukithiri kwa wizi wa kutumia silaha wa mifugo hali ambayo imekuwa ikisababisha uvunjifu wa amani.

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash, ametoa siku 14 kwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo kuyarejesha maeneo yote ya wafugaji yaliotegwa kwa ajili ya malisho yanayodaiwa kuuzwa na baadhi ya viongozi kwa wawekezaji.

“Natoa siku 14 kwa wakurugenzi wote wa Bagamoyo na Chalinze kuyarejesha maeneo yote yaliohodhiwa na kuuzwa na viongozi wa vijiji kwa wawekezaji Kwa maslahi Yao binafsi..suala hiloli limekuwa likichangia migogoro sana”amesema

Aidha Mkuu huyo wa wilaya, ameagiza taasisi ya kupambana na kuthibiti Rushwa TAKUKURU kufanya uchuzi na kuchukuliwa hatua za kisheria viongozi wote wa vijiji walihusika kuuza maeneo ya wafugaji yaliyopo katika mpango wa matumizi Bora ya ardhi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Possi, amesema migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ikichangiwa na ongezeko la mifugo, wafugaji kushindwa kufuata sheria pamoja na ongezeko la shughuli za kiuchumi na kijami.

Habari Zifananazo

Back to top button