Watengenezaji wa Precision Air kutua

 

MSEMAJI wa Serikali, Gerson Msigwa amesema timu ya wataalamu kutoka kampuni ya ATR-42 ambayo ndiyo watengenezaji wa ndege hiyo, wanatarajiwa kuwasili leo sambamba na wataalamu waliopo nchini kwa ajili ya matengenezo ya ndege hiyo.

“Watakuja na watengenezaji wa engine maana uchunguzi wa ajali za ndege unafanywa na pande tatu.” Amesema Msigwa

Akizungumza leo Novemba 8,2022 mjini Bukoba, Msigwa amesema kitengo maalumu cha uchunguzi wa ajali za anga kimeanza kazi na kifaa cha mawasiliano ambacho ni muhimu kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi kimepatikana.

“Niwahakikishie kwamba Serikali inaendelea kufanya juhudi za kuimarisha usalama katika usafiri wa anga katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Usafiri huu ndio usafiri salama. Katika usafiri wa kuaminika duniani ni usafiri wa anga,”amsema

Msigwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera na viongozi wengine kwa kazi kubwa ya kuhakikisha mara baada ya ajali hatua zinachukuliwa.

“Niwapongeze wananchi wa Bukoba hususani wavuvi ambao walijitokeza kwa haraka. Wamefanya kazi kubwa,” ameongeza Msigwa.

Habari Zifananazo

Back to top button