Watoa huduma bima za afya watakiwa kujisajili

DAR ES SALAAM: Watoa huduma za wanaotumia bima za afya wametakiwa kujisajili Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Ili kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hususani malipo ya fedha kutoka kwenye kampuni mbalimbali za bima.

Hayo yamesemwa leo Mei 23,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TIRA, Dk Baghayo Saqware, wakati akifungua mafunzo kwa wanachama wa Umoja wa Vituo vya Afya Binafsi Tanzania (APHFTA), ambapo amesema mamlaka hiyo imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa watoa huduma hao, ndipo Serikali imekuja na utaratibu wa kuwasajili.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa APHFTA Dk Berezy Makaranga, akizungumza katika semina hiyo ameishukuru serikali kwa kuanzisha utaratibu huo, huku akisema italeta ufanisi kwa watoa huduma bima za afya.

Meneja wa TIRA Kanda ya Mashariki, Zakaria Muyengi amesema kupitia semina hiyo watoa huduma watapewa mwongozo wa usajili na wanatarajia kujenga uhusiano na kutambuana vizuri katika utoaji huduma.

Habari Zifananazo

Back to top button