WATOTO 10 wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisha viungo katika kambi ya siku nne Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).
Kutokana na upasuaji huo kufanyika ndani ya nchi kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Ireland, kiasi cha Sh Milioni 180 hadi Sh mil 270 kimekoloewa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa kuhitimisha kambi hiyo, Mkurugenza Mtendaji wa MOI, Dk Respisius Boniface, amesema gharama ya kumtibu mtoto mmoja nje ya nchi ni Sh Milioni 20 hadi Sh mil 30 huku ndani ya nchi ikiwa ni Sh Milioni 1.3 hadi Sh mil. 3.
Amesema lengo la taasisi hiyo ni kuisaidia serikali na ,kuwasaidia wananchi kupata matibabu yote ambayo yanatakiwa bobezi ndani ya nchini.