Watoto 1,114 walawitiwa ndani ya mwaka mmoja

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, amesema jumla ya matukio 1,114 ya watoto kulawitiwa yameripotiwa kwa kipindi cha mwaka 2021 pekee.

Dk. Gwajima alitoa taarifa hiyo jana wakati akizungumuza kwa njia ya simu na wananchi wa mtaa wa Mwatulole, Kata ya Buhalahala mjini Geita walipokuwa katika mkutano wa hadhara.

Pia amesema watoto 5,899 wameripotiwa kubakwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa 2021, hali inayoashiria tishio kubwa la usalama wa mtoto na ongezeko la vitendo vya ukatili ndani ya jamii.

Waziri ameeleza hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao, wakidai kuhuzunishwa na taarifa ya kutochukuliwa hatua mtuhumiwa wa vitendo vya ulawiti aliyekamatwa mtaani hapo wiki iliyopita.

Dk. Gwajima ameahidi kuwasiliana na Inspekita Jenerali wa Polisi (IJP), pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi, ili kuhakikisha watuhumiwa wa vitendo vya ulawiti wanachukuliwa hatua kwa mjibu wa sheria.

Amewaomba wananchi kuendeleza ushirikiano wa kuwalinda watoto, kwani kuna matukio mengi ya vitendo vya ukatili yanaendelea kuwakumba watoto katika kipindi hiki.

“Waambieni watoto wakikutana na watu wasiowajua wakapewa zawadi, wanawafundisha tabia mbaya, wanawashika kifuani, wanawashika makalio, wanawashika sehemu za siri waambieni watoe taarifa.

“Unganeni mtangaze kwamba hili jambo halikubaliki, kilichofanywa na Rais Samia kuunda hii wizara ni jambo kubwa la kihistoria kukabili ukatili. Kwa hiyo wananchi wawe macho, wapaze sauti zao.”

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button