Watoto 200 kupatiwa matibabu bure MOI

DAR ES SALAAM: WATOTO 200 wenye matatizo ya mifupa na viungo wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi na upasuaji bure katika kambi maalum ya matibabu ya siku moja katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Kambi hiyo itafanyika Mei Mosi, 2024 ikiwa pia na lengo la kutafiti na kubaini magonjwa yanayowakabili watoto wadogo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upasuaji wa Mifupa na Tiba ya Majeraha Dk Antony Assey amesema magonjwa hayo yanahusiana na viungo mbalimbali kama magoti,nyonga,viwiko na uti wa mgongo.

“Watoto wengi wamekuwa wanakuja na matatizo ya muda mrefu japo huwa wanatibu hivyo tumetambua mwelekeo wa hayo matatizo hayafanyiki inavyopaswa na tumelenga kuwahudumia watoto 200 na matibabu hayo ni bure.

Kwa upande wale Meneja wa idara ya upasuaji mifupa na watoto,Dk. Bryson Mcharo amesema wamewaita watoto wa mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya karibuni ambao wana matatizo hayo ni wakati mzuri wa kufika hospitalini hapo kupata matibabu.

Daktari Bingwa bobezi wa upasuaji wa mifupa kwa watoto,Emannuel Lema amesema tatizo la watoto kuzaliwa na mguu vifundo ni kutokana na upungufu wa baadhi ya virutubisho kwenye uzazi hivyo mama kabla ya kupewa ujauzito apewe elimu ya kutosha.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button