Watoto 260 wauawa vurugu Palestina

MIONGONI mwa Wapestina 950 waliouawa katika vita inayoendelea huko Ukanda wa Gaza, imeelezwa 260 ni watoto, Wizara ya Afya Palestina imeripoti.

Wakati Palestina ikiripoti idadi hiyo ya vifo, mtandao wa Al-Jazeera umesema idadi ya waliouawa kwa upande wa Israeli imefikia 1,200.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imesema makombora yanayoendelea kurushwa na Israeli tangu Jumamosi kuelekezea nchini humo yameharibu makazi 22,600, vituo vya afya 10 na shule 48.

Zaidi ya watu 260,000 wameyakimbia makazi yao huko Gaza, huku zaidi ya 175,000 wakipata hifadhi katika shule 88 za Umoja wa Mataifa.

“Zaidi ya watu 263,934 huko Gaza wanaaminika kukimbia makazi yao,” Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu OCHA liliripoti, likionya kwamba “idadi hii inatarajiwa kuongezeka zaidi”.

Jeshi la Israel linasema kuwa limeharibu mfumo wa hali ya juu wa ufuatiliaji uliotengenezwa na Hamas ambao ulitumika kugundua ndege katika Ukanda wa Gaza.

“Katika miaka iliyopita, kundi hilo lenye silaha lilianzisha mtandao wa Kamera za hali ya juu, zilizofichwa ndani ya hita za jua Gaza, kwa lengo la kutambua na kufuatilia ndege angani.” jeshi liliongeza.

Jeshi hilo limesema limenasa miili ya wapiganaji 1,000 wa Hamas waliojipenyeza Israel mwishoni mwa juma.

Takriban wapiganaji 18 wameuawa msemaji mkuu wa jeshi la nchi hiyo Daniel Hagari aliwaambia waandishi wa habari, kulingana na gazeti la Israel Hayom.

“Hii inaashiria ukubwa wa shambulio hilo. Walikuwa na vifaa na tathmini za ushindi, sio kwa uvamizi bali kwa ushindi, “alisema.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *