WATOTO 335, 971 watambuliwa

Ni wanaoishi kwenye mazingira hatarishi

WATOTO 335, 971 wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wametambuliwa na serikali na kati yao Watoto wa kike 167,337 na Watoto wa kiume ni 168,634 huku migogoro ya ndoa 1,513 ilishughulikiwa.

Hayo yamesemwa leo Aprili 14, 2023 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma.

Amesema hadi kufikia Februari 2023 idadi hiyo ya Watoto wanaoshi kwenye mazingira hatarishi wameweza kutambuliwa na kupatiwa misaada mbali mbali ikiwemo chakula, mavazi, malazi, matibabuna elimu.

“Watoto 26,000 tumefanikiwa kuwaunganisha na familia zao na kuhakikisha watoto hao wanaishi kwa amani.”Amesema Kairuki

Aidha amesema, Tamisemi imeshughulikia migogoro ya kifamilia, ambapo hadi kufikia Februari, 2023 migogoro ya ndoa na familia 1,513 ilipokelewa katika ofisi za Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri na kati ya migogoro 1,513 iliyosajiliwa migogoro 868 ilifanyiwa usuluhisho kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri.

Amesema, migogoro 645 ilipewa rufaa kwenda mahakamani, ambapo migogoro 126 ilitolewa hukumu na migogoro 519 inaendelea na taratibu za Kimahakama.

Habari Zifananazo

Back to top button