Watoto 45 kufanyiwa upasuaji wa moyo

DAR ES SALAAM: WATOTO 45 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo yakiwemo matundu kwenye moyo, na matatizo ya mishipa ya damu kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Mending Kids lililopo nchini Marekani.

Kambi hiyo maalumu ya siku tano iliyoanza jana inatarajiwa kutoa matibabu ya upasuaji wa moyo wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab kwa watoto 25 na upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua kwa watoto 20.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2023 daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI, Stella Mongela amesema upande wa cathlab watoto 25 watapatiwa matibabu ya kuziba matundu mbalimbali yaliyopo katika kuta za moyo pamoja na kufungua mishipa ya damu iliyobana inayopeleka damu kwenye mapafu na kwenye mwili.

Amesema kupitia kambi mbalimbali zinazofanyika JKCI zimekuwa zikitoa fursa kwa madaktari wazawa kuendeleza ujuzi wao, kwani wamekuwa wakikutana na mabingwa waliofanya kazi kwa muda mrefu hivyo kuongeza ujuzi zaidi.

“Kambi ya wataalamu wa afya kutoka Shirika la Mending Kids ni moja ya kambi inayotupa nafasa wataalamu wa JKCI kujifunza mbinu mbalimbali za kutoa huduma bora za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto”, amesema.

Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Felix Shonyela amesema idara ya upasaji mkubwa wa moyo imepanga kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto kati ya watatu hadi wanne kila siku wakati wa kambi hiyo maalumu.

Dk Shonyela amesema wakati wa kambi maalumu watafanya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo yakiwemo matundu katika moyo na mishipa ya damu ambayo haiko sawa inayopeleka damu kwenye mapafu.

“Katika kambi hii tutaenda kurekebisha mishipa ya damu ambayo haiko sawa inayoelekea kwenye mapafu na kupelekea mishipa mingine inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu kuwa midogo, tunarekebisha mishipa hiyo ili damu iweze kwenda vizuri kwenye mapafu”, amesema Dk Shonyela.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Royal
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by. follow instructions on this website…….. http://Www.SmartCash1.com

FloellaRainbow
FloellaRainbow
1 month ago

★My buddy’s mother makes $90 per hour working on the computer (Personal Computer). She hasn’t had a job for a long, ( i99q) yet this month she earned $15,500 by working just on her computer for 9 hours every day.
Click and Copy Here══════►►► http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x