SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) limeeleza kwamba watoto 700,000 nchini Sudan wana uwezekano wa kukumbwa na aina mbaya zaidi ya utapiamlo mwaka huu, huku maelfu wakipoteza maisha.
“Matokeo ya siku 300 zilizopita yanamaanisha kuwa zaidi ya watoto 700,000 wana uwezekano wa kuteseka kutokana na aina mbaya zaidi ya utapiamlo mwaka huu,” James Elder, msemaji wa UNICEF,”
“UNICEF haitaweza kutibu zaidi ya watoto 300,000 kati ya wale ambao hawana ufikiwaji mzuri na bila msaada wa ziada. Katika hali hiyo, makumi kwa maelfu wanaweza kufa”.ameongeza
UNICEF inaomba Dola milioni 840 kusaidia zaidi ya watoto milioni 7.5 nchini Sudan mwaka huu.