WATOTO zaidi ya 93,218 walio chini ya umri wa miaka mitano, wanatarajia kupata chanjo ya polio itakayoanza kutolewa Septemba1 hadi 4 wilayani Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda ametoa rai kwa wazazi na walezi wilayani hapa, kuhakikisha wanawapeleka watoto vituo vya afya na hospitali mbalimbali kwa ajili ya kupata chanjo ya polio.
Amesisitiza chanjo hiyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya watoto, kwani haina madhara yoyote kwa watoto hao.
Naye Mratibu wa chanjo wilayani hapa, Hashimu Mtiti amesema chanjo hiyo ya polio ni salama haina madhara yoyote kwa watoto.
Amesema kampeni hiyo ya chanjo, itafanyika nyumba kwa nyumba na vituo vyote vya afya vilivyopo wilayani hapa.