Watoto Hospitali Mnazi Mmoja kupatiwa vifaa tiba

WATOTO wenye magonjwa yasiyoambukiza katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Dar es Salaam wanatarajia kupata vifaa tiba kutoka katika Taasisi ya ‘Runner Club ambayo’ inatarajia kuanzia mbio za Absa Dar City.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  jana jijini Dar es salaam,  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Godfrey Mwangingulu alisema mashindano hayo yanatarajia kukutanisha zaidi ya washiriki 3000.
Alisema mbio hizo zinatarajia kufanyika kati kati ya Mkoa wa Dar es salaam, kupitia katika vivutio mbalimbali ikiwemo kivutio kipya cha daraja la Tanzanite na vingine.
Mwanginguru alisema mbio hizo zitakuwa na majina tofauti, ambapo mbio ya Km 21 zitaitwa Absa, Km 10 zitaitwa Britam na Km  5 zitaitwa Alliance life Assurance.
“Mbio hizi zitakuwa za katikati ya mji, watu watakuwa wakiangalia vivutio vya hapa mjini.  Fedha zitasaidia watoto wa hospitali ya Mnazi mmoja na ndo sehemu mbio zitaanzia” alisema.
Akiongezea meneja biashara kutoka Jawa Masomo alisema wamejiunga na mbio hizo kwaajili ya afya kwa wafanyakazi wao na wateja. Alisema katika mashindano hayo washiriki watapata fedha taslim, medali pamoja na ringi za mkononi zinazoashiria mshiriki amemaliza kazi.

Habari Zifananazo

Back to top button