Watoto milioni 2.8 wakabiliwa utapiamlo Afrika
WATOTO milioni 2.8 wanakabiliwa na utapiamlo katika nchi za Afrika, huku umaskini, vita na mabadiliko ya tabianchi vikitajwa kuendelea kuongeza idadi ya watu wenye utapiamlo wa kupindukia.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), utapiamlo unatarajiwa kuongezeka kutokana na athari za kiuchumi za janga la Covid -19 na vita vinavyoendelea nchini Ukraine, ambavyo vinaharibu mnyororo wa ugavi na kupandisha bei ya nafaka, mbolea na nishati.
Kwa mujibu wa ripoti ya Hali ya Dunia ya Usalama wa Chakula na Lishe ya 2022 iliyotolewa hivi karibuni, idadi ya watu duniani kote ambao hawawezi kumudu lishe bora iliongezeka kwa milioni 112 na kukaribia kufikia hadi bilioni 3.1, ikionesha athari za kupanda kwa bei ya vyakula katika uwezo wa kumudu milo kamili.
Nchi za Mali, Chad, Burkina Faso, Niger, Nigeria, Ethiopia, Kenya na Somalia zimetajwa kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha utapiamlo kutokana na kukabiliwa pia na upungufu wa maji kutoka milioni 9.
5 hadi milioni 16.2