“Watoto wa kike wapewe nafasi wanaweza”

DAR ES SALAAM: Shirika la Mwanamitindo Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na Msichana Initiative, Sema na Tai storytelling for Social Change wamezindua kampeni ya kumlinda mtoto wa kike walioiita Ajenda ya Msichana.

Kampeni hiyo inakwenda sambamba na Kumpatia mtoto wa kike elimu kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike inayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka ili kusherehekea mafanikio na uwezo wa msichana.

Akizungumza na Habari leo Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative waandaaji wa jukwaa la msichana 2023, wamesema kuwa wanafanya kazi za kutetea haki kwa wasichana ili kuondoa vikwazo vilivyopo mbele yao katika kuzifikia ndoto zao.

“Bado kuna tamaduni na mila ambazo isivyo bahati zinawachukulia watoto wa kike kujikita na majukumu yao ya kijinsia kuliko uwezo wao.”amesema

Afisa Mawasiliano na Ushirikiano wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation Allah Sheve amesema mtoto wa kike ni nguzo ya familia na maendeleo kuangalia mazingira rafiki ya kusoma kwa bidii hivyo anatakiwa kupata mazingira wezeshi, katika familia na jamii kumfanya aweze kubaki shule mfano kuwa na choo safi katika kupata hedhi salama.

Habari Zifananazo

Back to top button