‘Watoto wa kiume hali ni mbaya wakumbukwe’

Askofu Dk Stanley Hotay.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Stanley Hotay, amesema katika jamii sasa mtoto wa kiume amesahauliwa, huku hali yake ikiendelea kuwa mbaya katika maandalizi yake ya kuwa baba wa familia.

Askofu Dk Hotay akizungumza na HabariLEO amesema maadili sasa yameporomoka na hali ya watoto wa kiume ni mbaya, wanafanyiwa uhalifu na wanaanguka katika mitihani.

“Watoto wa kiume sasa hawafanyi vyema shuleni wameangushwa na mtoto wa kike amelindwa, lakini ataishi nchi ya peke yake?” Anahoji na kuongeza:

Advertisement

“Watoto hawapatikani kwa jamii moja naomba sasa tutetee mtoto wa kiume maana kilio kimeongezeka .

“Sio tu shuleni hawafanyi vizuri, lakini uhalifu umeongezeka, ninaomba Mungu atusaidie ukatili katika familia ukomeshwe sisi viongozi wa dini tuwe mstari wa mbele, kuna maneno yapo hata kwenye dini ukatili upo.”

ASkofu Dk Hotay ameomba kwa Mungu awasaidie viongozi wa dini kuwa kioo,chumvi na nuru katika jami,i kwani woga na wasiwasi ni riba ya kitu ambacho mtu hatakimiliki maisha yake yote.

15 comments

Comments are closed.

/* */