Watoto wa kiume wawezeshwe pia

WAKATI dunia ikiendeleza kasi katika kuchagiza uwezashaji kwa watoto wa kike, ombwe la kuwaangalia na watoto wa kiume limeonekana kuwa na umuhimu mkubwa.

Hayo yamebainishwa hivi karibunina Meneja mradi wa afya ya uzazi kwa vijana balehe wa shirika la World Vision Tanzania, Mwivano Malimbi hivi karibuni wakati Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Harjit Sajjan alipotembelea Shirika la Baba Watoto linalotekeleza mradi huo.

Malimbi amesema uwezeshaji watoto wa kike katika nchi unakwenda vizuri sana. Changamoto zilizobaki ni chache na himilivu.

“Kundi la watoto wa kiume ni kundi ambalo limeachwa sana na kwa sasa kundi hili limekua likikabiliwa na changamoto kubwa ukilinganisha na mabinti,”

Amesema kundi la watoto wa kiume limeachwa sana, akibainisha moja ya sifa ya mradi wa Accelerated Hope and Development for Urban Adolescent (AHADI) unaotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali unalenga kuwashika mkono makundi yote ya vijana kwanzia umri wa balehe.

Aliainisha baidhi ya mashirika wanayoshirikana nayo kutekeleza mradi wa AHADI ikiwemo Baba Watoto Organization na Kiwohede ambao wao sasa wamejikita kuhakikisha uelewa wa masuala ya afya ya uzazi kwa vijana balehe na Medicine Du Monde ambao wanawafikia vijana waraibu wa dawa za kulevya.

Pia, World Vision inafanya kazi na Kibaha Institute of Business ambao wao wamejikita katika kukuza uchumi kwa vijana kwenye nyanja kuu ambazo ni kuhakikisha wanajiingiza kwenye ujasiriamali na wale vijana waliokosa fursa za kuingia kwenye mfumo rasmi wa elimu, basi nao wapate fursa ya kuingia kwenye mfumo wa elimu ambao watachagua,” amesema.

Amesema vijana watakaoamua kujikita kwenye biashara basi ni wajibu shirika hilo kuhakikisha wanapata elimu sahihi na wanakuwa na tabia chanya zitakazowajengea kujiamini na wao pia kuaminika hasa zinapokuja nyakati za mikopo, kupitia mradi huo wa Ahadi.

Kufuatia hali hiyo, wazazi na walezi wa watoto walio nje ya shule wameshauriwa kuwahimiza watoto wao kujiunga na programu ya AHADI kwa ajili ya kuboresha tabia zao.

Mradi huo ulioanza kutekelezwa Januari mwaka huu umewafikia vijana karibu asilimia 28 ya walengwa kwa mkoa wa Dar es Salaam, “Dodoma umefikia asilimia 35 na ni wito wetu kwa wazazi na walezi wenye vijana ambao wako nje ya shule, wale wenye miaka 10 hadi 19 kuwahamasisha kujiunga na vukindi hivi vinavyozingatia ujenzi wa maadili.”
Amesema katika utekelezaji wa mradi huo kuna vikundi mbalimbali ambavyo vinaongeza uelewa na kuchochea mabadiliko ya tabia chanya kwa vijana balehe hasa katika wilaya nne za Mkoa wa Dar es Salaa, ikiwemo Temeke, Kinondoni, Ilala na Ubungo na kwa Dodoma unatekelezwa katika wilaya Dodoma Jiji.

Malimbi ametaja changamoto kubwa wanayokutana nayo ni za mfumo ambao unasaidia kuboresha uchumi kwa vijana, ambayo haiwabebi vijana walio chini ya umri wa miaka 18 kwa sababu sheria inawatambua kama watoto.

“Kwa hiyo twende katika mifumo mbalimbali na katika sera ambazo haziruhusu hawa vijana kupata viwezeshi vya kuwaimarisha katika uchumi, tuone sasa ni wakati wa kuwafikiria pia, katika mikopo, wanatakiwa kigezo cha kwanza wawe na Nida ambayo pia ina kigezo cha umri.

“Ni vyema na Serikali ione sasa kuna haja ya kuangalia hili kundi maalumu lililo nje ya shule na bado wamekosa fursa ya kwenda kwenye mifumo ya elimu,” amesema.

Amesema Halmashauri si changamoto sana ila shida ni vijana kuaminika, uaminifu kwa vijana umekuwa ni mdogo.
Mkurugenzi Baba Watoto Organization, Mgunga Mwamnyenyelwa amesema wanafanya shughuli zao kwa ufadhili wa World Vision Tanzania kupitia Serikali ya Canada lengo ni kuwasaidia viaja walio ndani na nje ya shule ili waweze kuhimili changamoto zilizopo hasa zinazohusiana na afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa ujumla wake.

Katika kituo cha Baba Watoto baadhi ya shughuli za mradi huo zinafanyika, ikiwa ni kata moja lakini kuna kata tatu na wamekuwa wakifanya miradi hiyo kwa zaidi ya miaka 20.

“Baba Watoto imekuwa ikifanya shughuli hiyo kwa zaidi ya miaka 20 na ukiingia kwenye kituo hiki utakuta kuna michoro mingi ya sanaa (naionyesha), ikimaanisha vijana wengi wamewezeshwa kiuchumi kwa kupitia sanaa, wamepata ufundi na ujuzi wa sanaa hasa sarakasi na ukiona kuna matukio mengi jijini Dar es Salaam, wasanii wakiwa 10 wanafanya sarakasi, basi hapo angalau watatu wanatoka hapa,” amesema Mgunga.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Money
Money
1 month ago

Taulo za kike na VITU VYA KWETU

Tangazo.PNG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x