Watoto wadai dereva alipuuza ushauri wa kuvuka mto

ARUSHA: Mashuhuda na watoto waliokuwa katika basi la wanafunzi la Shule ya Ghati Memorial ambalo limesombwa na maji na kusababisha kifo cha watoto watano huku wengine watatu kutojulikana walipo wamedai dereva wa gari hilo alitahadharishwa kutopita katika korongo hilo la Engosengiu hata hivyo alicheka na kupuzia tahadhari hiyo.

Watoto hao ambao wamenusurika katika ajali hiyo, wamesema katika mahojiano na waandishi wa habari kwenye Kituo cha Afya cha Murriet kuwa Matroni alimzuia dereva kujaribu kuvuka katika eneo hilo hata hivyo alipuuza na hatimaye walisombwa na maporomoko ya maji.

Glory Daniel, Mtoto mwenye umri wa miaka 8 amesema “Uncle Lukuman (Lukuman Daniel) amesababisha yote haya.”

Glory na wenzake wawili pamoja na Mwalimu wao ambaye pia ni Matroni wapo katika Kituo cha Afya cha Murriet. Watoto hao wametambuliwa kwa majina ya Preygod Daniel (10), Rose Immanuel (10) na Mwalimu Annastazia Immanuel (27).

 

Habari Zifananazo

Back to top button