Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wasaidiwa

OFISA Tarafa Kata ya Elerai, Titho Cholobi kwakushirikiana na wadau mbalimbali wametoa msaada  pampasi, maziwa ya kopo, taulo za majimaji katika wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo, Cholobi amesema ameguswa kama mwana jamii kuhamasisha wenzake kutoa misaada huo, ili kusaidia watoto hao wenye uhitaji

Amesema wameshrikiana kuhakikisha wanatoa misaada kwa watoto njiti, ambao wengine wazazi wao wamekufa baada ya kujifungua

“Msaada huu ni kwa ajili ya watoto hawa na nimepata huzuni baada ya kuona kuna watoto wamefiwa na wazazi wao, hivyo tumejichanga kama jamii kusaidia watoto hawa, ” amesema na kuongeza kuwa msaada huo una thamani ya Sh milioni 2.

Naye Muuguzi Mkuu wa Hospitali  ya Rufaa ya Mount Meru, Simphorosa Silalye ameshukuru kwa msaada huo kwa watoto wenye uhitaji maalum na kuomba jamii kujitokeza kusaidia watoto hao.

“Tunashukuru kwa msaada huu wa maziwa, pampas na tishu maalumu za kuwafutia  watoto hawa wenye mahitaji maalum, tunaomba na wengine wajitokeze kusaidia, ” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button