Watoto wasumbua wizi Ikungi

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amesikiliza na kupatia ufumbuzi kero za wananchi wa Puma, wilayani Ikungi na kuagiza wakuu wa wilaya katika Mkoa huo kufanya hivyo kwa sababu amebaini wananchi wanateseka.


Miongoni mwa malalamiko yaliyowasilishwa kwake kupitia mkutano wa hadhara uliyofanyika leo Januari 19, 2023 kwenye Kata ya Puma, ni kukithiri kwa wizi ambao kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Samuel Mbihaji, unafanywa na watoto wadogo wenye umri usiozidi miaka 15.

Awali Joram Zacharia alisema wizi huo mara nyingi unafanyika kwenye makazi yao usiku na imefikia kiwango cha kutokuwa na uhakika wa kuamka salama.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mbihaji,


Naye Mbihaji amesema hivi karibuni kwa kushirikiana na kituo cha polisi kijijini hapo walifanya msako wa wezi, asilimia 75 ya waliokamatwa walikuwa watoto ambao waliachiwa baada ya polisi kusema hawakuwa na pa kuwapeleka.


“Wazazi tukiwaita wanasema tufanye tunavyotaka wao wamewashindwa, sasa hatujui cha kufanya,” amesema Mbihaji

Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Ikungi, Suzan Kidiku amemuomba Mbihaji kutoishia kituo cha polisi kijijini hapo badala yake afikishe suala hilo kwake litashughulikiwa.

“Upo mchakato wa kushughulikia watoto wanaokulia katika mazingira ya hivi, tutashirikisha maafisa ustawi wa jamii, watafikishwa mahakamani,” amesema Kidiku.

Serukamba ametaka viongozi wa kijiji, kata, polisi na mamlaka nyingine zichunguze kwa kina suala hilo kwa sababu inawezekana watoto wanatumika.

Ameagiza ifikapo Alhamisi, wiki ijayo apelekewe taarifa ya kilichobainika au maendeleo ya kazi hiyo.

OCD wa Ikungi, Suzan Kidiku

Habari Zifananazo

Back to top button