Watoto wawili wa familia moja wafariki kwa kuungua na Moto

KATAVI: Watoto wawili wa kike Florida Frowin (miaka 3) na Felician Frowin (Mwaka mmoja na nusu) wameteketea kwa kuungua na moto hadi kufa ndani ya nyumba yao huku mmoja akiokolewa na wananachi waliowahi kufika eneo la tukio katika mtaa wa Tulieni Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Wakizungumzia tukio hilo Adam Rehan, Phoibe Elias na Faustin Kalele ambao ni majirani wamesema moto huo ulikua mkali lakini kwa jitihada za wananchi walijitahidi kufanya uokoaji licha ya juhudi zote waliambulia kumuokoa huyo mtoto mmoja.

Baba wa watoto hao, Frowin Digili kwa amesema wakati tukio linatokea hakuwepo nyumbani na taarifa alizipata akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na majirani huku mama wa watoto hao akiwa sokoni.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Geofrey Mwambungu, ambaye ni mkuu wa oparesheni kutoka Jeshi la Zimamoto mkoani Katavi, amesema tukio hilo la moto limetokea majira ya asubuhi na limeteketeza mali zote zilizokua ndani huku watoto wawili wakifariki na mmoja akiokolewa na wananchi waliowahi kufika katika tukio hilo.

Amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Sambamba na hilo Jeshi la Zimamoto limesisitiza wananchi kujenga nyumba kwa kufuata taratibu na maelekezo ya serikali ili kuondokana na changamoto za kimiundombinu zinazopelekea kutofika haraka kwenye tukio.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button