Watu 10 wafariki katika mlipuko wa gari la mafuta
Watu 10 wamethibitishwa kufariki, huku wengine 27 wakijeruhiwa baada ya Lori la mafuta kulipuka katika mji wa Boksburg nchini Afrika Kusini leo.
Diwani wa Ekurhuleni Simon “Sijawahi kuona kitu kama hiki hapo awali na siwezi kuamini kiwewe ambacho kimetokea kama hii siku moja kabla ya Krismasi,” amesema Simon.
Simon amesema uchunguzi umeanza ili kufahamu sababu za gari hilo kulipuka. “Lazima kuwe na uchunguzi wa kina kuhusu jinsi lori linalobeba LP Gas linaweza kwenda chini ya daraja la kiwango cha chini. Kwa kawaida malori haya hayaruhusiwi kufanya hivyo,” ameongeza.
Aidha imefahamika kuwa kati ya watu hao, watu wazima sita na watoto wawili ndiyo waliopoteza maisha
Mlipuko huo ulitokea baada ya lori, mali ya kampuni ya Infinity Gas, lililokuwa limebeba LP Gas, kwenda chini ya daraja la reli kwenye Barabara ya Hospitali, karibu na Hospitali ya Kumbukumbu ya OR Tambo.