TAKRIBANI watu 12 wameuawa katika vurugu zilizotokea ndani ya Uwanja wa El Salvador ambapo mashabiki wa soka walikusanyika kutazama mechi kati ya FC Alianza na Club Deportivo FAS. Taarifa ya polisi nchini humo imeeleza.
“Tuna matokeo mabaya ya waathiriwa 12, tisa ambao wako hapa uwanjani na wengine watatu ambao tumearifiwa wako katika vituo tofauti vya hospitali,” Mkurugenzi wa Polisi wa Kitaifa (PNC) Mauricio Arriaza amewaambia waandishi wa habari leo.
Polisi walisema ripoti za awali zinaonyesha mashabiki waliojaribu kuingia uwanjani katika mji mkuu wa San Salvador wa Amerika ya Kati kutazama mechi kati ya FC Alianza na Club Deportivo FAS.
“Kulikuwa na milango miwili tu iliyofunguliwa katika uwanja mzima,” shabiki mmoja aliambia La Prensa Grafica. “Watu waliokuwa nje walitaka kuingia kwa nguvu, na wote wakatuangukia.”
Shabiki mwingine, Sandra Argueta, alisema watoto na wazee waliathiriwa na lango lililoanguka kwa kupigwa teke “ili kupata hewa kwa sababu kulikuwa na watu wengi na tulikuwa tukikosa hewa”.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa El Salvador, Juan Carlos Bidegain amesema wahudumu wa kwanza wa huduma ya ulinzi wa raia walikuwa kwenye eneo la tukio na kuwahudumia watu walioathiriwa na tukio hilo.
Mechi hiyo ilisitishwa huku wahudumu wa dharura wakiwaondoa watu kutoka uwanjani hapo, ambapo mamia ya maafisa wa polisi na wanajeshi walikusanyika huku ving’ora vya gari la wagonjwa vikilia.