Watu 14 wafa, maelfu wamekwama mafuriko Somalia

WATU 14 wamekufa na zaidi ya 47,000 kukwama kwenye matope na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Jubbaland nchini Somalia na kusababisha mafuriko, Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya Kibinadamu limeeleza.

Mvua kubwa iliyonyesha mwezi uliopita imeongeza kiwango cha maji kwenye mto Juba na kusababisha mafuriko katika maeneo ya mito ya jimbo hilo.

“Katika Wilaya ya Luuq, watu 2,400 wamenaswa katika eneo lililozingirwa na maji,” iliongeza taarifa hiyo.

Advertisement

Juhudi za mamlaka na washirika wa uokoaji zinaendelea kuwaondoa wenyeji waliokwama.

Waziri wa Habari wa Somalia alisema mafuriko hayo ambayo pia yaliathiri majimbo ya Hirshabelle na Kusini Magharibi, yamesababisha uharibifu mkubwa.

Aliomba uungwaji mkono, akiongeza kuwa hali ni mbaya.

3 comments

Comments are closed.

/* */