Watu 14 wafa mafuriko India

IDADI ya vifo imeongezeka na kufikia 14 baada ya mafuriko katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Sikkim nchini India kukumbwa na mvua kubwa na kusababisha mafuriko.

Watu 26 pia walijeruhiwa na wengine 102, wakiwemo wanajeshi 23, waliripotiwa kutoweka, maafisa walisema Alhamisi.

Kwa mujibu wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa (IMD) mvua hiyo ilinyesha kwa ukubwa wa 40.9 mm kwa siku mbili Jumanne na Jumatano ikielezwa kuwa ni mara tano ya kiwango cha kawaida cha 8.6mm.

Imeelezwa kuwa mvua hizo zimepasua Ziwa la Lhonak la mwinuko wa juu, ambalo liko chini ya barafu katika vilele vinavyozunguka mlima wa tatu kwa urefu duniani, Kangchenjunga.

Mvua hiyo pia imeharibu ukuta wa maji unaoendeshwa chini ya mkondo, na kuongeza mto ambao tayari umevimba na mvua za masika, kuharibu bwawa, kufagia nyumba na madaraja, na kusababisha “uharibifu mkubwa”, serikali ya jimbo la Sikkim ilisema.

Barabara zilikuwa “zimeharibiwa” na madaraja 14 yalikuwa yamesombwa na maji kando ya kingo za mto Teesta.”ilieleza taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button