Watu 17 wafa maporomoko ya udongo Lisala
WATU 17 wameuawa katika maporomoko ya udongo huko DR Congo.
–
Maafa hayo yalitokea usiku wa kuamkia Jumapili karibu na kingo za mto Congo, katika mji wa Kaskazini wa Lisala, mji mkuu wa Mkoa wa Mongala.
–
Wanawake saba, wanaume saba na watoto watatu chini ya miaka mitano walikufa.
–
Walizikwa siku hiyo hiyo kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kuwaweka katika hifadhi ya maiti ya eneo hilo, Afisa wa Lisala Désiré Koyo aliambia BBC.
–
Gavana wa Mongala, César Limbaya, alituma rambirambi kwa familia zote za waliofariki.
–
Ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo , wakati ambapo bendera zitakuwa zinapepea nusu mlingoti.