WATU 17 wamekufa na zaidi ya 208 kujeruhiwa baada ya lori lililowabeba kuanguka katika jimbo la Niger nchini Nigeria, kikosi cha usalama barabarani kimeeleza.
–
Msemaji wa kikosi hicho, Bisi Kazeem amesema ajali hiyo imetokea Jumanne kijiji cha Takalafia eneo la Serikali ya mtaa wa Magama jimboni hapo.
–
“Waathiriwa waliojeruhiwa wamehamishwa hadi Hospitali Kuu ya Kantagora kwa matibabu ya haraka, waliofariki wapo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo hiyo,” Kazeem alisema.
–


3 comments