Watu 170 wauawa mashambulizi Burkina Faso

TAKRIBANI watu 170 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji vitatu nchini Burkina Faso, mwendesha mashtaka wa umma anasema.

Aly Benjamin Coulibaly aliomba mashahidi kusaidia kupawata waliowashambulia vijiji vya Komsilga, Nordin na Soro.

Coulibaly alisema alikuwa ameanzisha uchunguzi kuhusu mashambulizi ya kijiji kimoja katika jimbo la Yatenga Februari 25, 2024. Haikujulikana ni kundi gani lilikuwa nyuma ya mashambulizi hayo.

Wakuu wa jeshi walionya juu ya kuongezeka kwa hatari ya mashambulizi ya wanamgambo ikiwa ni pamoja na mashambulizi kwenye maeneo ya mijini.

Habari Zifananazo

Back to top button