WATU 20 wamefariki katika ajali ya basi Kusini mwa Ethiopia, wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa, mamlaka eneo hilo imeeleza.
Ajali hiyo imetokea Mkoa wa Oromia nchini humo, katika Wilaya ya Teltale, karibu na mpaka wa Kenya.
Watu 18 kati ya waliojeruhiwa wamepata majeraha mabaya.
–
Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka mji mdogo uitwao Milami kuelekea soko la kijiji karibu.
Comments are closed.