TAKRIBANI watu 24 waliokuwa wakielekea Ulaya wamekufa baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Pwani ya Kaskazini mwa Senegal, maofisa wa eneo hilo wanasema.
Gavana Alioune Badara Samb aliambia shirika la habari la AFP miili yao ilipatikana siku ya Jumatano.
Mashuhuda wanasema meli hiyo ilibeba zaidi ya watu 300.
Gavana huyo amesema haijulikani ni watu wangapi walikuwa kwenye mashua hiyo. Watu kadhaa walionusurika na walifanikiwa kufika ufukweni.
Rais Macky Sall alionyesha alituma salamu za pole kwa familia za waathirika.