Watu 31 wafa mafuriko Somalia

IDADI ya waliokufa kutokana na mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini Somalia imefika 31, mamlaka imeeleza katika taarifa yake.

Tangu mwezi Oktoba mwaka huu, zaidi ya watu 500,000 wamekimbia makazi yao, Waziri wa Habari, Daud Aweis alieleza katika taarifa yake huko Mogadishu. “Mafuriko pia yamesababisha uharibifu wa miundombinu katika Mkoa wa Gedo, Kusini mwa Somalia.”alisema Daud Aweis.

Advertisement

Ofisi ya U.N. ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetoa Dola million 25 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko hayo.

“Wakati hatua zote zinazowezekana za maandalizi zikifuatiliwa, mafuriko ya kiwango hiki yanaweza tu kupunguzwa na kutozuiliwa,” OCHA ilisema, ikipendekeza “onyo la mapema na hatua za mapema” kuokoa maisha.

3 comments

Comments are closed.