TAKRIBANI watu 63 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa kufuatia moto kuwaka katika jengo la ghorofa katikati mwa jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
–
Msemaji wa Huduma za Dharura za Johannesburg, Robert Mulaudzi amesema moto huo umezuka leo asubuhi na kuteketeza jengo lililoko katikati mwa jiji la biashara, na idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka, huku miili 63 ikipatikana kutoka eneo hilo kufikia sasa.
–
Taarifa za hivi punde miili 63 imepatikana na 43 kujeruhiwa,” Mulaudzi alisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa X.
–
“Bado tunaendelea na shughuli ya utafutaji na uokoaji.” alisema.
–
Mtoto mmoja alikuwa miongoni mwa waliofariki, na wale waliojeruhiwa walikuwa wakipokea matibabu katika “vituo mbalimbali vya afya,” alisema.
–
“Zaidi ya miaka 20 katika huduma, sijawahi kukutana na kitu kama hiki.” Mulaudzi aliongeza.


2 comments