IDADI ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa kipindupindu nchini Zambia imeongezeka hadi 700, linasema shirika la matibabu la Médecins Sans Frontières (MSF).
Namba hiyo ni kubwa kuwahi kurekodiwa.
Ilianza katika mji mkuu, Lusaka, mwezi Oktoba na tangu wakati huo imeenea katika majimbo yote ya Zambia na kuwaambukiza watu zaidi ya 19,000.
MSF imesema kipindupindu kinatibika kwa urahisi kwa kuongezewa maji mwilini lakini bila uangalizi mzuri mtu anaweza kufa.
“Ugonjwa huu husababishwa na maji machafu, hivyo upatikanaji wa maji safi ya kunywa ni muhimu ili kuuzuia kuenea zaidi”.
Imeeleza taarifa yao