Watu 72 kati ya 100 hutumia chumvi ya kawaida Mtwara

WATU 72 kati ya 100 sawa na asilimia 72 ya Kaya katika Mkoa wa Mtwara hutumia chumvi ya kawaida ambayo haina madini joto, Mkuu wa Mkoa Kanali Ahamed Abbas amesema na kutaka uchunguzi wa kimaabara wa chumvi zinazozalishwa na kusambazwa mkoani humo.

Akizungumza katika hafla ya itiaji saini Afua za Lishe Mkoani humo, Kanali Abbas amesema: “Pamoja na kupungua kwa viwango vya utapiamlo, tafiti zimebainisha kuwa asilimia 72 ya Kaya katika mkoa wetu hutumia chumvi zisizo na madini joto ya kutosha.”

Amesema uchunguzi huo utasaidia kubaini endapo kuna uwepo wa madini joto kulingana na miongozo ya serikali na kama hakuna sheria zichukuliwe kwa wahusika.

“Hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wazalishaji au wauzaji wa chumvi ambao watabainika kusambaza chumvi isiyo na madini joto ya Kutosha,” amesema.

Kwa mujibu wa wa Shirika la Afya Duniani, jamii isiyotumia chumvi yenye madini joto ya Kutosha ipo katika hatari ya madhara kama kuvimba Kwa tezi la shingo, kuharibika Kwa mimba , watoto kuzaliwa na uzito pungufu.

Madara mengine ni kuzaa mtoto njinti , mtoto kufia tumboni au kuzaliwa na kufariki mara tu ya kuzaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button