Watu 75 wauawa vurugu Sudan Kusini

TAKRIBANI watu 75 wamepoteza maisha ndani ya wiki mbili baada ya kuzuka ghasia kati ya jamii hasimu eneo la Abyei mpaka wa Sudan na Sudan Kusini.

Akitoa taarifa hiyo, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, Nicholas Haysom ametoa wito kwa serikali nchini humo kuchuguza hali ya wasiwasi, lakini kutotumia nguvu kusuluhisha.

Kumekuwa na mapigano yanayoendelea kati ya jamii za Ngok na Twic kuhusu rasilimali huko Abyei.

Mapema wiki hii jeshi la Sudan Kusini lilishutumiwa na kiongozi wa eneo hilo kwa kuratibu mashambulizi na vijana wapinzani wenye silaha madai ambayo wanajeshi wameyakanusha.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button