Watu 83,000 wanahitaji msaada Rufiji

PWANI: MUU wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele amesema wilaya yake ina  jumla ya kata 13 kati ya hizo kata 12 zimeathirika na mafuriko.

Meja Gowele amesema hayo leo Aprili 9, 2024 katika ziara maalum ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, alipotembelea waathirika wa mafuriko Rufiji.

Amesema, tayari kata tisa zimefanyiwa tathimini na kubaini kaya 23,000 zimeathirika na mafuriko hayo na watu 88,000 wanahitaji msaada wa huduma muhimu ikiwemo makazi, chakula na huduma za afya.

“Mbali ya makazi ya wananchi kukumbwa na mafuriko, pia hekta 33,930.24 za mazao zimeathiriwa,”amesema Meja Gowele.

Amesema katika maafa hayo ya mafuriko watu wawili wamepoteza maisha ambao ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 na mtoto wa mwaka mmoja.

“Wananchi walioathirika tumewahamisha kwenye madarasa ya shule, hata hivyo tunalazimia kuendelea kuzifunga shule na wanafunzi ambao wapo madarasa ya mitihani tunawafanyia utaratibu wa kuwahamisha shule nyingine za wilaya ya jirani,”amesema.

Amesema shule ya Mhoro ambayo imefanywa kambi ya wananchi tayari nayo imeshazingirwa na maji.

Habari Zifananazo

Back to top button