Watu bilioni 2 wanakazi zisizo rasmi

WATU milioni 473 duniani wanakosa fursa ya kupata kipato kupitia ajira, huku watu milioni 205 wasio na ajira wanakidhi mahitaji ya soko la ajira na wapo tayari kupokea ajira muda wowote.

Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inasema kuwa Watu bilioni 2 kati ya wale walioajiriwa wana kazi zisizo rasmi, maana yake ni kwamba wana uwezekano mdogo sana wa kuwa na haki kazini, uhuru wa kupaza sauti au kufurahia faida za mfumo wa ulinzi wa kijamii ikiwemo  Bima ya Afya, Bima ya Ajira, na Fao la Uzeeni

Ripoti hiyo pia inasema watu milioni 214 wako katika ajira lakini hawawezi kujinasua kutoka katika umaskini wa kupindukia yaani wao na familia zao wanaishi chini ya dola 1.9 za Kimarekani kwa Siku

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button