Watu kadhaa wahofiwa kufa ajali ya boti Cape Verde

WATU kadhaa wamekufa na wengine 38 kuokolewa katika ajali ya boti Cape Verde. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeonya kuwa makumi ya watu wanahofiwa kufariki.

Hayo yanajiri baada ya watu 63 kuhofiwa kufa wakati mashua ya wahamiaji iliyotoka Senegal mwezi Julai ilipopinduka kutoka Cape Verde.

Huduma za dharura zilipata mabaki ya watu saba, msemaji wa IOM, Safa Msehli ameliambia shirika la habari la AFP, huku watu wengine 56 wakiaminika kupotea.

“Kwa ujumla, watu wanaporipotiwa kupotea kufuatia ajali ya meli, hudhaniwa kuwa wamekufa,” alisema.

Watu 38 walionusurika ni pamoja na watoto wanne wenye umri wa miaka 12 hadi 16, aliongeza Msehli.

Mashua ya wavuvi iliondoka Senegal mwezi mmoja uliopita, kulingana na ripoti za vyombo vya habari huko Cape Verde, taifa la kisiwa kilicho karibu kilomita 620 kutoka pwani ya Afrika Magharibi.

Habari Zifananazo

Back to top button